Mfanyabiashara ya Dawa za Kulevya ‘Rocco Morabito’ Atoroka Gerezani na Wenzake

0
70

Nguli wa biashara ya dawa za kulevya nchini Italia, Rocco Morabito na wafungwa wenzake watatu wametoroka gerezani nchini Uruguay.

Rocco na wenzake walitoroka kupitia tundu kwenye paa la Gereza Jumapili ya wiki iliyopita.

Baada ya kutoroka walitekeleza wizi katika makazi ya wanaoishi jirani na gereza kwa mujibu wa taarifa ya iliyotolewa na Mamlaka ya mambo ya ndani ya nchini Uruguay siku ya Jumatatu.

Rocco Morabito mwenye umri wa miaka 52 alikuwa akisubiria kupelekwa nchini Italia baada ya kuishi Uruguay miaka 13 kwa jina bandia.

Rocco alikuwa miongoni mwa watuhumiwa wa kundi la kiharifu la Ndrangheta mwaka 2017 kabla ya kukamatwa kusini mashariki mwa Uruguay.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here