Nadia Mukami Aijongea Valentine’s Day Bila Faraja Ya Mpenzi

0
76

Mwimbaji kutoka Kenya, Nadia Mukami amedai kuwa kuelekea Februari 14 2020 siku ya wapendanao anaendelea kujipumzisha bila mpenzi ‘Single’ baada ya kuvunjika kwa ahusiano yake kwa muda sasa.

Akiwa mubashara kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nadia aligusia kuwa alichopitia kilimsukuma kuandika wimbo wake ‘Lola’ ft #Masauti ulioandikwa kwa simulizi ya usaliti.

Akisikiliza wimbo wake ‘Lola’ alisema “This is a song I wrote about the story of my life…it been long since I fall in love with someone else…watu tuna-celebrate valentine pekee yetu” Alisema Nadia.

Pia Nadia aliongeza kuwa Mashabiki wategemee kazi kadhaa kutoka kwake zikiwemo kolabo za nyimbo alizowashirikisha mastaa wa muziki kutoka Tanzania, Marioo na Maua Sama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here