Director Zed Benson aliyeandaa na kuongoza video za muziki za msanii Jux nchini China ameeleza hofu yake juu ya Virusi tishio vya Corona na sababu za kurejea kwake nchini Ghana.

Akipiga Stori na #DizzimOnline, Zed Benson alisema kuwa hali ya tishio inayosabishwa na Corona Virus hata kupelekea idadi kubwa ya vifo haihusiani na yeye kurejea kwake nyumbani Ghana.

Director Zed alieleza kuwa alirejea nchini Ghana kwasababu za kikazi ikiwemo kufungua kampuni yake ya kuandaa video iliyopewa ‘Songhai Pictures’ kwani nchini China alienda kimasomo na tayari amemaliza hilo.

Pia Zed aliongeza kuwa bila hofu kabisa ana mpango wa kurejea China kufanya manunuzi ya vifaa vipya na vya kisasa katika kuboresha uandaaji wa kazi za video chini ya kampuni yake hiyo.

Hata hivyo Zed kati ya video za muziki zake, Jux alizoongoza ni ‘Nitasubiri’ na ‘Sisikii’ ambapo katika Mahojiani alimalizia kuwa ana mpango wa kutembelea Tanzania kwa nia ya kufanya kazi na baadhi ya wasanii tofauti na Jux.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here