Pierre Nkurunziza

Leo Mei 20, 2020, Unafanyika uchaguzi Mkuu wa kwanza nchini Burundi wa kumchagua Mrithi wa Rais wa nchini hiyo Pierre Nkurunziza.

Wananchi wenye vigezo vya kushiriki uchaguzi nchini humo wanapiga kura kumchagua Rais na wawakilishi wengine wakiwemo wabunge licha ya kuwepo kwa changamoto ya janga la Ugonjwa wa Corona.

Uchaguzi huu wa Burundi unawakutanisha wagombea saba katika nafasi ya Urais ya Pierre Nkurunziza ambaye hatawania tena nafasi hiyo baada ya kukaa madarakani kwa miaka 15.

Baada ya uchaguzi huu wa kumpata mrithi wa Rais Nkurunziza kumalizika na matokeo kutamgazwa inatarajiwa hali ya mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Tume ya taifa ya Uchaguzi nchini humo, imesema wapiga kura zaidi milioni 5 wanatarajia kushiriki uchaguzi huo na matokeo yanatarajiwa kuanzia Mei 25.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mtandao wa BBC Swahili, Mitandao ya kijamii nchini haifanyi kazi huku wapigakura wakiendelea na zoezi la Uchaguzi mkuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here