Msanii wa muziki wa rap na Muigizaji kutoka Tanzania, Hennesseyy ameachia rasmi video ya wimbo utakaotumika kama ‘Sound track’ kwenye filamu yake ijayo kwa jina ‘Speed’.

Sound track hiyo ambayo Hennessyy anasikika akichana, video yake imeongozwa na Director Mims nchini Tanzania Baada ya Audio kutayarisha kikamalifu kwa usimamizi wa Spacious Music na Producer Paul Loops.

Hata hivyo inaelezwa kuwa Mfululizo wa baadhi ya matukio yanayooneakana kwenye video ya wimbo huo ni sehemu ya maudhui ya filamu hiyo ijayo ambayo Hennesseyy pia ameigiza.

Taarifa za kuaminika zikieleza kuwa Filamu hiyo itaingia sokoni hivi karibuni kwakuwa tayari wako katika hatua za mwisho za kuikamilisha..

Filamu hiyo imeandaliwa nchini nchini Tanzania kwa asilimia kubwa kwa ushirikiano wa waigizaji na waandaaji maarufu nchini, lakini pia waandaaji wa Filamu hiyo wako katika mpango w kushirikiana na wadau wengine kutoka nje ya nchini katika muendelezo wake.

Moja ya Cover ya Filamu hiyo Ijayo

Itazame video ya Soudn Track hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here