Viongozi hao wamepata maambukizi baada ya kutangamana na jopo la ngazi ya juu la kukabiliana na virusi hivyo nchini humo.

Taarifa kutoka nchini Sudani Kusini zinaeleza kuwa Makamu Rais wa kwanza wa nchi hiyo Riek Machar na mke wake Angelina Teny wamepimwa nairusi vya Corona.

Dkt. Machar amesema kwamba yeye na mke wake ambaye pia ni waziri wa ulinzi, wamepata maambukizi baada ya kutangamana na jopo la ngazi ya juu la kukabiliana na virusi hivyo nchini humo.

Machar amesema atajiweka karantini siku 14 pamoja na kuwa hana dalili zozote na hali yake ya afya iko sawa.

Adha Wengine waliothibitishwa kuambukizwa ni walinzi kadhaa na wafanyakazi ambapo mpaka sasa Sudan Kusini imerekodi waathirika 236 na vifo vinne.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here