Rapper kutoka Tanzania, Venance William a.k.a Mabeste ameachia wimbo wake mpya, ‘Back Off’ unaozungumzia sehemu ya Maisha yake ya Mahusaino Mpaka kutoa talaka kwa Mkewe.

Wimbo wake huu mpya, Mabeste amezungumzia alichowahi kueleza kuwa, kuvunjika kwa mhusiano yake na Lisa Karl Fickenscher kisha mrembo huyo kuingia kwenye mahusiano na mtu wa karibu wa Rapper huyo ‘Pax Pyne’ hali hiyo iliyompa wakati mgumu kiasi cha kutamani ‘kufa’.

Mabeste

Kwenye uandishi rapper Mabeste anasikika kwenye michano akisema “kuji suicide yoh! nafeel heartless…kuna marafiki fisi…wamemanga manzi yangu tafuna mifupa…”.

“majamaa nuksi, matendo yao fix…familiar cheating/ tunafeel guilty, marafiki fisi…wamemanga manzi yangu tafuna mifupa…” ikihisiwa kuwa anazungumzia kuachana na Aliyekuwa Mkewe Lisa.

Katika kumbukumbu za maisha ya Rapper Mabeste ni kuwa Oktoba, 2016 alichukua maamuzi ya kufunga ndoa takatifu na aliyekuwa mpenzi wake Lisa Karl Fickenscher ambaye waliachana baada ya kudumu kwenye ndoa yao kwa miaka mitatu.

Mabeste na Lisa Enzi za Mahusiano yao ‘Siku ya Ndoa’

Katika mapenzi yao kwa takribani Miaka 8 kuanzia uchumba mpaka Ndoa, Mabeste na Lisa walifanikiwa kupata watoto wawili, Kedrick na Kaylyn. Lisa Mwaka huu na Mpenzi wake wa sasa ambaye alikuwa Boss wa kibiashara wa Mabeste, Pax Pyne wamefanikiwa kupata mtoto wa kike aliyepewa jina ‘Kylie Pax’.

Itakumbukwa kuwa Mabeste na aliyekuwa Mkewe Lisa, kila mmoja alijichora tatoo ya jina la mwenzake ili kuonyesha jinsi gani wawili hao wanapenda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here