Home News Rapper Tekashi69 Aingia Kwenye Rekodi Mpya Baada Ya Kutoka Jela

Rapper Tekashi69 Aingia Kwenye Rekodi Mpya Baada Ya Kutoka Jela

0
51

Rapper kutoka Marekani, Tekashi69 au 6ix9ine ameingia kwenye rekodi ya ‘Instagram Live’ ya kuwa Nyota wa muziki wa rap aliyetazamwa na watu wengi zaidi ‘Live’ kwa kufikisha watu Milioni 2+.

https://www.instagram.com/p/B_8IGyVDKa-/

Tekashi ambaye jina lake halisi ni Daniel Hernandez mwenye umri wa miaka 24, ameingia kwenye rekodi hiyo kupitia live chat yake ya kwanza kupitia ukurasa wake wa Instagram, ikiwa ni wiki kadhaa tangu aruhusiwe kutoka jela kutokana na sababu za kiafya.

Tekashi kwasasa anaendelea kutumikia kifungo cha nje cha miezi 4 iliyobaki kwenye hukumu yake ya miaka 2. Pia Tekashi ameachia wimbo wake wa kwanza kwa jina ‘Gooba’ ukiwa ndo wimbo wake wa kwanza kuuachia tangu atoke jela.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here