Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda ametangaza punguzo la asilimia 80 ya bei leo Mei 21, 2020, na kuyataja maduka yaliyoridhia kufanya biashara ya kuuza nguo kwa punguzo hilo.

Maduka hayo ni pamoja na Mr Price, Red Tag ya Mlimani City, Vunja Bei, maduka ya nguo yaliyopo City Mall pamoja na maduka mengine yaliyopo Posta, Kariakoo, Kinondoni na Sinza.

Lakini wamiliki wa maduka hayo nao, hawakuwa nyuma kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya manunuzi, huku wakimpongeza RC Makonda kwa kuwapigania wananchi ili kuhakikisha wanapata mavazi mazuri kwa bei nafuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here