Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Raia wote wa Uganda kuanzia umri wa miaka 6 watapewa barakoa bure kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Rais wa nchini humo, Yoweri Museveni amesema itakuwa lazima kuvaa barakoa(Mask) kwa kila mtu awapo kwenye maeneo ya umma.

Mbali na hilo Rais Museven aliongeza kuwa usafiri wa umma utarejeshwa kwa huduma Juni 2 baada ya watu kugawiwa barakoa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here