Staa wa wimbo ‘Utaniua’, Yangy kutoka nchini Kenya ameutupia wimbo ‘Quarantine’ wa wasanii kutoka lebo ya WCB Wasafi katikati ya mfuatano wa maudhui ya kuutangaza wimbo wake mpya.

Kupitia Insta Story yake, Yangy aliamua kutupia video ya vijana waliokuwa wakiucheza wimbo huo wa WCB, katikati ya mfululizo maudhui ya kuutangaza wimbo wake ‘Utaniua’ hali iliyohisiwa kuwa amenogewa na wimbo ‘Quarantine’.

Hata hivyo Yangy anendelea kufanya vziuri na wimbo wake huo ‘Utaniua’ ambao kwa muda mfupi umepata mapokezi mazuri Zaidi kwenye vituo mbalimbali nchini Kenya na kwenye Mitandao ya kijamii.

Itazame video ya wimbo wake hapa chini.