Msanii wa muziki  kutoka nchini Kenya anayefanya kazi za muziki wake chini ya lebo ya muziki iitwayo ‘Levels Creative’, Shazzie Kemz amekutana kisanaa na mwimbaji Nyota na mkali wa wimbo ‘Utamu’ ft Rapper Young Lunya , Haitham Kim wa nchini Tanzania.

Shazzie Kemz

Wawili hawa katika kuunganisha nguvu ya Sanaa Afrika Mashariki, walikutana kwenye kazi ya pamoja kwa jina ‘Dhamana’ chini ya utayarishaji Lizer Classic, wimbo ambayo video yake imetoka rasmi kupitia mtandao wa Youtube na unapatikana kwenye platforms mbalimbali duniani kote.

Haitham Kim

Kutoka Kenya, Msanii Shazzie Kemz anakuwa kati ya wasanii wachache waliofanya kazi iliyowakutanisha wasanii kutoka Afrika Mashariki chini ya Procuder Lizer Classic mwenye mtiririko mzuri wa kutayarisha hits kubwa Afrika na Nje ya Afrika kutoka Wasafi Records.

Lizer Classic na Diamond Platnumz

Tazama video ya wimbo huo hapa chini.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here