Msanii wa muziki kutoka Burundi mkali wa Afro-Beats anayefanya kazi zake nchini Marekani, maarufu kama ‘Mt Number One’ ameachia video rasmi ya wimbo wake mpya kwa jina, ‘Don’t Go’.

Mt Number One

‘Don’t Go’ ni wimbo wake wa pili rasmi kutoka sambamba na video kwa mwaka 2020, baada ya kufanya vizuri katika chati mbalimbali za redio na Tv, na wimbo wake ‘Nduhura’ uliotoka mwezi Januari mwaka huu.

Itazame video ya wimbo wake huo mpya hapa chini.

Mt Number One anayeaminika kuwa kati ya wanaofanya vizuri kisanaa anatajwa kati ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanaofanya kazi zake nje ya Afrika Mashariki, akiwa ni mwenye kuipeperusha vyema bendera ya taifa la Burundi.

Pia, Mt amekuwa na rekodi nzuri ya kuachia wimbo pamoja na video yake bila kuhofia gharama kwakuwa alishanukuliwa akieleza kuwa, muziki ni sehemu kubwa ya maisha yake, hivyo atawekeza kwa namna awezavyo kwa lengo la kupata kazi nzuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here