Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania Mwenye makazi yake nchini Marekani, Blaise Platii-Na ameachia rasmi album yake ya kwanza.

Blaise mwenye umri wa miaka 22, aliachia album hiyo yenye nyimbo 8 inayokwenda kwa jina ‘African Love’, iliyoingia sokoni rasmi Agosti 27 mwaka huu.

Kwenye album hiyo, Blaise amemshirikisha mwimbaji mmoja pekee wa kike aitwaye Lizzie Baby kwenye nyimbo mbili, ambazo ni  ‘Controlla’ na ‘Give Me Love’.

Mwimbaji Blaise akiwa na Mwanamitindo

https://music.apple.com/us/album/african-love/1530069565?uo=4&app=itunes&at=1001lry3&ct=dashboard

Blaise anaamini kuwa hatua yake ya kuachia album yake hiyo, ni mwanzo mzuri wa kufikia ndoto zake kama mwimbaji tajika Afrika kutokana na kukua kwa teknolojia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here