Nyota wa muziki wa Dancehall, Thabani Ndlovu maarufu kama Buffalo Souljah amesaini mkataba na kampuni ya biashara ya muziki na burudani ya nchini Jamaika, Natural Bond Entertainment.

Mkataba huu mpya kati nyota huyo wa wimbo ‘No man bigger than God’ na Natural Bond utahusika zaidi na kutangaza na kusimamia muziki wake hasa katika Visiwa vya Karibi ‘Jamaika’.
Buffalo Souljah mzaliwa wa Zimbabwe mwenye makazi yake nchini Afrika kusini, sasa kwa mkataba huo anendelea kuimarisha uhusiano wake na kampuni hiyo maarufu kwa kukuza kazi za wasanii wa reggae/dancehall ukanda huo.
Katika mahojiano ya ‘The Herald Arts’, Jerome Elvie amabye ni mtayarishaji na mmiliki kampuni hiyo, alieleza kupendezwa sana na kazi za Buffalo.

Hata hivyo Buffalo Souljah tayari ameachia album yake mpya,’UNITY’, ikiwa ni album yake ya sita kuingizwa sokoni.
UNITY ALBUM BY BUFFALO SOULJAH
Album hiyo ya Buffalo imeingia sokoni rasmi Sepetemba 18 2020.
Mfuate Buffalo Souljah kwenye mitandao ya kijamii.
Twitter: www.twitter.com/buffalosouljah1
Facebook: www.facebook.com/buffalosouljah
Instagram: www.instagram.com/buffalosouljah1