Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta ametajwa katika tetesi za kuiacha Aston Villa na kutimkia Uturuki.

Mitandao mbalimbali ya nchini Uturuki imeripoti kuwa Mtanzania Mbwana Ally Samatta anaweza kutambulishwa wakati wowote kuanzia sasa kama Mchezaji mpya wa miamba ya soka nchini humo, Fenerbahce akitokea Aston Villa ya Uingereza.

Mbwana Samatta

Nahodha Mbwana Samatta mwenye umri wa miaka 27 anatajwa katika tetesi hiyo ya usajili ikiwa ni baada ya miezi kadhaa ya kuitumikia klabu ya Aston Villa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here