Mtayarishaji nyota wa nchini Marekani, Swizz Beatz amejitokeza kueleza juu ya alichofanya Diamnd Platnumz kwenye Album ya Saba ya Alicia Keys, ‘ALICIA’.

Mkali Kasseem ‘Beatz’ Dean anaeleza kuwa Diamond awaeleweshe mashabiki kuwa kwenye wimbo ambalo ameshirikishwa alifanya kulingana na maamuzi yake jambo ambalo baadhi ya mashabiki walionesha kuwa Diamond amewapa kiasi kidogo cha burudani.

Diamond anasikika akitumia lugha ya taifa ya Tanzania(Kiswahili) katika uandishi wake kwenye wimbo ‘Wasted Energy’ kutoka kwenye Album hiyo ambapo aliimba kwa sekunde zisizozidi ‘30’ mwisho wa wimbo.

Hata hivyo Swizz aliongeza kuwa alichofanya Diamond ni sehemu ya kwanza tu huku kauli hiyo ikiashiria kuwa kuna uwezekano kukawa na kazi nyingine ambayo Swizz au Alicia Keys kushirikiana na Diamond Platnumz.

Album hiyo ya Alicia inaendelea kufanya vizuri hata kushikilia nafasi za juu Duniani katika chati mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here