Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, umeeleza kufurahishwa na hatua ya kushirikishwa kwa nyota Diamond Platnumz kwenye album mpya ya Alicia Keys, ‘ALICIA’.

Diamond Platnumz

Kupitia mtandao wa twitter wa Ubalozi huo, ulieleza kuwa ni furaha yao kuona Alicia Keys wa nchini Marekani kumshirikisha Diamond kutoka Tanzania kwenye wimbo ‘Wasted Energy’ kwenye album hiyo.

Alicia Keys

Hata hivyo Ujumbe huo wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania uliombatana na link ya wimbo huo wa kutoka kwenye Mtandao wa Youtube, uliutaja wimbo huo kuwa ni wimbo wa moto.

Ujumbe wa Ubalozi huo kwenye Ukurasa wa Twitter

 

Usikilizew eimbo huo hapa chini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here