Msanii wa muziki wa kizazi kutokea nchini Kenya, K Rhyme Classic ameleza kuvutiwa na mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii nchini humo, Azziad Nasenya na kuweka wazi hilo bila kuficha ficha.

Akipiga story na Dizzim Online, K Rhyme alieleza kuvutiwa na uzuri wa mrembo huyo hata kueleza kuwa awali uongozi wa lebo yake ya ‘Usanifu Music’ ulipanga atokee kwenye video ya wimbo wake mpya, ‘Melo’.

“Navutiwa sana na urembo huyu mrembo wetu Azziad wa hapa hapa nyumbani na ujue Usanifu Music ilikuwa wamtafute atokee kwenye video ya huu wimbo wangu ‘Melo’”.

Lakini mambo yakawa Mengi na muda ukawa unaenda wakaamua tuifanya haraka na itoke kwakuwa kazi ni nyingi naamini kuna kazi ambayo itafaa yeye kutokea” Alisema K Rhyme.

VIDEO YA WIMBO ‘MELO’ WA K RHYME HAPA CHINI.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here