Msanii wa muziki wa Rap kutokea Sydney, Australia, Simorix Jenerali a.k.a The General, amewaomba watanzania kulinda amani na kuitumia haki ya kimsingi ya kumchagua kiongozi atakayelinda amani ya Nchini ya Tanzania.

Simorix Jenerali a.k.a The General

Msanii huyo mzaliwa wa nchini Tanzania, anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Magu Chuma’ aliwasihi watanzania kudumisha amani na upendo katika kuchukua maamuzi ya kumchagua kiongozi Bora katika uchuguzi mkuu utakaofanyika kesho, Oktoba 28 2020.

Mimi ni mtanzania tena mtanzania mzalendo, hivyo siwezi kufurahi nikiona kunatokea hali ya ukosefu wa amani katika nchini yangu hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Nawaomba watanzania wenzagu wailinde amani ya nchini yetu kwa kumchagua kiongozi zatakayezingatia hilo ili uchaguzi huu umalizike kwa amani na utulivu” Alisema The General.

Itazame video ya wimbo wake huo ‘Magu Chuma’ hapa chini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here