Home Uncategorized Wizkid ahairisha ujio wa album yake, ‘Made In Lagos’

Wizkid ahairisha ujio wa album yake, ‘Made In Lagos’

0
21
Nyota wa muziki kutokea nchini Nigeria,Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu kama Wizkid amehairisha mpango wa kuachia album yake ya nne, ‘Made In Lagos iliyotarajiwa kutoka rasmi  ‘Oktoba 15 2020’.
Wizkid alikuwa kwenye mpango wa kuachia album yake hiyo na moja ya sababu za kuihairishwa kwake ni kutokana na hali ya maandamano inayoendea nchini humo.
Maandamano hayo yaliliyodumu kwa siku kadhaa sasa, yanafanyika kushinikiza mamlaka za juu za usalama kukomesha hali ya unyanyasaji, uonevu na mauaji vinaoelezwa kutekelezwa na baadhi ya maafisa usalama wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Ujambazi nchini humo, ‘S.A.R.S’.
Wizkid katika ujumbe wake kwenye ukurasa wake wa Instangram, pia aliomba radhi kwa atakaowakwaza kwani hali ilivyo nchini humo imemlazimu kuchukua maamuzi hayo.
Hata hivyo Wizkid alieleza kuwa, kuachia album kwa kipindi hiki ni hesabu mbaya kulingana na hali inayoendelea ya mambo muhimu ya kijamii nchini humo kutafutiwa ufumbuzi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here